Thursday, September 13, 2012
HISTORIA YA MAISHA YANGU.
Katika historia ya maisha yangu nilipata mahangaiko mengi sana kutafutiwa shule ya viziwi.Na pia uwenzo wa wazazi ulikuwa mdogo sana.Hadi nikafikia miaka 12 ndiyo nikaanza kusoma shule ya viziwi nilipo kuwa nasoma sikuwa na kitu chechote zaidi nikuomba msaada kwa majirani.pamoja na kwa marafiki zangu.nilisoma kwa uvmilivu sana hadi nilipomaliza shule ya msingi niliomba kazi ya muda mfupi neema crafts nikafanya kwa muda mfupi tu.Baada ya kusubiria matokeo ya mitihani nikashitukiwa kuwa nimefauru nikachaguliwa kwenda kusoma shule ya secondari malangali.Baada ya hapo nikaanza kuangahika kutafuta ada ya shule.nilihangaika kwamuda wa mwezi mmoja nikafanikiwa kupata msaada kwenye kanisa la Anglikana.Nilipo pata msaada huo nilienda kuendelea na masomo ya secondari . Baada ya miaka miwili nikapata matatizo nika shindwa kuendelea na masomo.Nikaandika barua fupi na kupeleka kwa msaidizi wangu.Nikapewa majibu kuwa nikafanye kazi Neema Crafts.Nilipoanza kufanya kazi neema crafts naapo majukumu ya nyumban yaliwa mazito hadi sasa bado sijasonga vizuri.lakin na mshukuru Mungu kwa kunipa ujasiri.
Subscribe to:
Posts (Atom)